Serikali ya Tanzania imethibitisha jana kuwa watu watano wamekufa mkoani Kagera kutokana na ugonjwa wa virusi vya homa ya Marburg. Kabla ya taarifa hiyo kutolewa kulikuwa na hofu kubwa miongoni mwa raia. Sikiliza mahojiano kati ya Bakari Ubena na Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma katika Wizara ya Afya nchini Tanzania, Dokta Tumaini Haonga.