1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaVenezuela

Watu 32 wafariki Venezuela kufuatia tetemeko la ardhi

25 Juni 2026

Watu wasiopungua 32 wamefariki na zaidi ya 700 wamejeruhiwa baada ya matetemeko mawili makubwa ya ardhi kuikumba Venezuela, kwa mujibu wa taarifa za Kaimu Rais Delcy Rodríguez.

https://p.dw.com/p/5G2Ss
Venezuela Catia La Mar 2026 | Tetemeko la ardhi | Delcy Rodríguez
Wafanyakazi wa dharura wakisimama karibu na majengo yaliyoharibiwa kufuatia tetemeko la ardhi huko Catia La Mar, jimbo la La GuairaPicha: Federico Parra/AFP

Serikali imeonya kuwa idadi ya vifo na majeruhi inaweza kuongezeka kadri juhudi za uokoaji zinavyoendelea.

Hakukuwa na takwimu kamili kutoka jimbo la Guaira, eneo la pwani ya Bahari ya Karibi ambalo limeathirika vibaya zaidi.

Kiongozi huyo wa Venezuela amelieleza jimbo hilo kama "eneo la maafa", akisema matetemeko hayo ya ardhi yaliyotokea mfululizo ni janga la kitaifa, na serikali imetangaza hali ya hatari.

Wafanyakazi wa uokoaji wanaendelea kuwatafuta manusura wanaohofiwa kufunikwa chini ya vifusi vya majengo yaliyoporomoka.

Huduma za treni kote nchini humo zimesimamishwa, na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Caracas umefungwa kutokana na uharibifu mkubwa uliotokea.