1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington.Brown awasili kwa mazungumzo na Bush.

30 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBdu

Waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown amewasili nchini Marekani kwa mara ziara yake ya kwanza ya mazungumzo na rais wa nchi hiyo George W. Bush tangu kuingia madarakani mwezi uliopita.

Kabla ya ziara hiyo , Brown amesema kuwa Marekani itabaki kuwa mshirika muhimu wa nchi yake.

Taarifa hiyo imefuatia matamshi ya mjumbe mwandamizi katika baraza la mawaziri la waziri mkuu Brown kuwa Uingereza haitakuwa tena na Marekani kama watoto pacha walioungana mwili katika sera zao za mambo ya kigeni.

Viongozi hao wawili wanatarajiwa kukutana kwa chakula cha usiku katika nyumba ya mapumziko ya rais ya Camp David kabla ya mazungumzo rasmi kuanza leo Jumatatu.

Majadiliano yaliyokwama ya shirika la biashara la dunia WTO pamoja na mzozo wa kiutu katika jimbo la Darfur nchini Sudan yanatarajiwa kuwa katika ajenda muhimu.