1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin anatumai kushinda muhula mwengine madarakani

Sylvia Mwehozi
15 Machi 2024

Raia nchini Urusi wameanza zoezi la kupiga kura katika uchaguzi wa rais utakaofanyika kwa siku tatu ambao unatazamiwa kuongeza muhula wa Rais Vladimir Putin kwa miaka sita zaidi.

https://p.dw.com/p/4dcW7
Urusi | Putin
Rais anayetetea kiti chake madarakani Vladimir PutinPicha: Evgenia Novozhenina/REUTERS

Uchaguzi huo unafanyika katikati mwa ukandamizaji mkubwa wa wapinzani ambao pia umeteteresha uhuru wa vyombo vya habari, kuyanyima nafasi makundi ya kutetea haki za binadamu na kumpatia rais Putin udhibiti kamili wa mfumo wa kisiasa.

Raia watapiga kura kuanzia leo hadi Jumapili katika jumla ya maeneo 11 yaliyo na tofauti ya masaa na vilevile kwenye mikoa iliyonyakuliwa kinyume cha sheria ya Ukraine. Mkaazi huyo wa Urusi anayo matumaini na uchaguzi wa leo. 

Raia wa Urusi wapiga kura ya rais

"Sasa tunamchagua rais wa nchi kwa siku zijazo, na ninapendelea kile kinachofanyika sasa, ningependa kiendelee na hata kuboreshwa, kwa sababu kizazi kipya lazima kiishi kwa amani na maelewano kwamba kusiwe na vita", alisema mmoja ya wakaazi wa Urusi.

Waangalizi wana matarajio kidogo kwamba uchaguzi huo utakuwa huru na wa haki.