1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Wapiganaji watatu Wakipalestina wauwawa na jeshi la Israel

22 Mei 2023

Wapiganaji watatu wa Kipalestina wameuwawa usiku wa kuamkia Jumatatu katika uvamizi uliofanywa na jeshi la Israel katika Ukingo wa Magharibi.

https://p.dw.com/p/4Retm
Palästina | Israelische Angriffe auf Gaza Stadt
Picha: Belal Salem/APA Images/ZUMA Press/picture alliance

Taarifa iliyotolewa leo na wizara ya afya ya Palestina imethibitisha juu ya kuuliwa watu hao iliowataja majina yao na umri.

Shirika la habari la AFP limejaribu kuwasiliana na jeshi la Israel hata hivyo halikupatikana kutowa tamko lake kuhusiana na mkasa huo. Jeshi la mashahidi la Al Aqsa ambalo ni tawi la wapiganaji la chama cha rais Mahmoud Abbas, Fatah kwenye taarifa yake limesema wapiganaji watatu waliouwawa ni wanachama wake.

Mashahidi wamesema  jeshi la Israel lilivamia nyumba chungu nzima Ukingo wa Magharibi kuwasaka  watu waliotakiwa na jeshi hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Pakistan Anschlag in Quetta
Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW
Nenda ukurasa wa mwanzo