1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapiga kura nchini Mali waidhinisha mabadiliko ya katiba

24 Juni 2023

Tume ya uchaguzi nchini Mali imesema jana kuwa raia nchi humo wameidhinisha kwa wingi mabadiliko ya katiba. Mabadiliko hayo yalipitishwa kwa asilimia 97 na raia walioshiriki katika kura hiyo.

https://p.dw.com/p/4T0hH
Mali | Verfassungs-Referendum
Picha: Baba Ahmed/AP/dpa/picture alliance

Maafisa wa uchaguzi wamesema idadi ya wapiga kura katika kuamua mabadiliko hayo mnamo Jumapili iliyopita ilikuwa chini ya  asilimia 39.4 ya watu milioni 8.4 waliojiandikisha kupiga kura.

Soma zaidi:Mali wapigia kura rasimu mpya ya katiba

Uongozi wa kijeshi nchini humo na mamlaka za kikanda ambao kwa pamoja waliunga mkono kura hiyo ya maoni wamesema hatua hiyo itaiwezesha Mali kufanya uchaguzi Februari 24 mwakani na kurejea kwenye utawala wa kiraia. Hata hivyo, wapinzani wanasema mabadiliko hayo yatawezesha jeshi kusalia madarakani baada ya uchaguzi mwaka ujao.