1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapalestina wauwawa kwenye ghasia za Ukingo wa Magharibi

Saumu Mwasimba
13 Machi 2024

Machafuko mabaya yaliyotokea usiku wa kuamkia leo, yamesababisha Wapalestina kadhaa kuuwawa katika Ukingo wa Magharibi.

https://p.dw.com/p/4dTfI
Afisa wa Israel
Askari wa Israel Ukingo wa MagharibiPicha: Ammar Awad/REUTERS

Machafuko mabaya yaliyotokea usiku wa kuamkia leo, yamesababisha Wapalestina kadhaa kuuwawa katika Ukingo wa Magharibi huku polisi ya Israel ikisema mpalestina mmoja amewashambulia kwa kisu watu wawili na kuwajeruhi katika kituo cha ukaguzi kilichoko karibu na mji wa Jerusalem, kabla ya kupigwa risasi leo Jumatano.

Machafuko yameongezeka katika eneo hilo la Ukingo wa Magharibitangu kundi la wanamgambo la Hamas kuishambulia Israel Oktoba 7 na kuchochea vita vikubwa kati ya nchi hiyo na kundi hilo la Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa wizara ya afya ya mamlaka ya Wapalestina takriban watu 427 wameuwawa Ukingo wa Magharibi kufikia sasa. Mvutano kati ya Israel na Wapalestina mara nyingi huongezeka makali wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu kwa Waislamu wa Ramadhan, na hasa kutokana na mabishano juu ya matumizi ya eneo takatifu,ulikojengwa msikiti wa Al Aqsa, mjini Jerusalem.

Wakati huohuo Israel imesema malori sita ya msaada yameruhusiwa kuingia Gaza kupitia Kaskazini jana usiku katika wakati shinikizo la jumuiya ya Kimataifa limeongezeka kuitaka nchi hiyo iruhusu msaada zaidi wa kibinadamu kuingizwa Gaza.