1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanafunzi kadhaa wauawa baada ya kupigwa risasi Urusi

11 Mei 2021

Wanafunzi kadhaa wameripotiwa kuuawa, baada ya mtu mwenye silaha kuwafyatulia risasi kwenye skuli yao kwenye mji wa Kazan nchini Urusi.

https://p.dw.com/p/3tEle
Russland Kasan Schießerei im Gymnasium Nr. 175
Picha: Maksim Bogodvid/Sputnik/dpa/picture alliance

Kwa mujibu wa mashirika ya habari ya Urusi, wanafunzi watano na mwalimu mmoja hadi sasa wamethibitika kupoteza maisha.

Madaktari, waziri wa afya, pamoja na magari 11 ya kubebea wagonjwa yametumwa kwenye skuli hiyo.

Shirika la habari la TASS linasema mshambuliaji mmoja, mvulana wa miaka 17, anashukiwa kuhusika na anashikiliwa na polisi, na mshambuliaji mwengine ameuawa kwenye makabiliano na polisi.
 

Mamlaka za mji wa Kazan zimewaondosha wanafunzi wote waliobakia kwenye eneo hilo.

Kawaida, matukio ya ufyatuaji risasi kwenye maeneo ya umma ni machache nchini Urusi kutokana na sheria kali za kudhibiti unuzuzi na matumizi ya silaha.