1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Wakaazi wa Rafah waingiwa wasiwasi kufuatia agizo la Israel

6 Mei 2024

Raia wa Kipalestina walioko katika mji wa Rafah, wameelezea kukata tamaa wakati Israel ikidondosha vipeperushi vinavyowataka kuondoka kwenye mji huo kwa usalama wao, kabla ya mashambulizi ya ardhini.

https://p.dw.com/p/4fYZm
Mzozo wa Mashariki ya kati | Rafah
Wakaazi wa Rafah wajiuliza "tutakwenda wapi?"Picha: Abed Rahim Khatib/dpa/picture alliance

Mapema Jumatatu, jeshi la Israel lilizielekeza familia za Kipalestina zilizoko mashariki mwa Rafah, kujiandaa kuondoka kabla ya kufanya mashambulizi kwenye mji huo ulio mpakani na Misri.

Lakini wakati wakimbizi wengi wasio na makaazi wakifungasha virago tayari kuondoka, mamlaka katika Ukanda wa Gaza unaoendeshwa na Hamas, zilisema kwamba tayari Israel inayalenga maeneo maalum ambayo yameamuriwa watu kuondoka upande wa mashariki mwa Rafah.

Kulingana na jeshi la Israel, maeneo ambayo watu wameelekezwa kwenda yana hospitali, mahema na huduma nyinginezo muhimu ikiwemo vyakula na vifaa vya matibabu. Lakini mashirika ya kiutu yanasema maeneo hayo yana msongamano mkubwa wa watu.