1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wajumbe wa Marekani na Iran waanza mazungumzo Islamabad

11 Aprili 2026

Waakilishi wa Marekani na Iran wameanza leo mazungumzo ya amani mjini Islamabad nchini Pakistan kutafuta makubaliano yenye lengo la kumaliza mzozo wa Mashariki ya Kati.

https://p.dw.com/p/5C1ms
Pakistan Islamabad 2026 | JD Vance na Shehbaz Sharif
Naibu Rais wa Marekani JD Vance (kushoto) na waziri mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif (kulia) kabla ya mazungumzo ya amani na IranPicha: Pakistan's Prime Minister Office/AFP

Wajumbe hao wawili walianza mazungumzo ya ana kwa ana leo alasiri chini ya usimamizi wa Pakistan baada ya siku ya mashaka na usiri ambao ulizua uvumi iwapo wajumbe hao watakutana au la.

Kumekuwa na uvumi wa siku nzima ulioashiria kuwa  ujumbe wa Iran huenda usikae na ule wa Marekani  na kwamba ni ujumbe tu ungetumwa kupitia wapatanishi, Pakistan.

Chanzo kimoja cha ulinzi cha Pakistan kilichozungumza kwa masharti ya kutotajwa jina, kimeliambia shirika la habari la dpa kwamba mazungumzo hayo yameanza vizuri.

Haya yanajiri huku jeshi la Israel likisema leo kuwa limeshambulia zaidi ya shabaha 200 za Hezbollah nchini Lebanon ndani ya saa 24 zilizopita.