Wajerumani wazungumzia uchaguzi wa Marekani | Matukio ya Kisiasa | DW | 04.11.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

UJERUMANI

Wajerumani wazungumzia uchaguzi wa Marekani

Asilimia 86 ya wajerumani walioulizwa kuhusu uchaguzi wa Marekani wameonesha kama wangepewa nafasi wangempigia kura Hillary Clinton kuwa rais wa Marekani huku asilimia 4 tu wameonekana kumuunga mkono Donald Trump.

Theresa Scholz mstaafu mwenye miaka 85 ambaye pia amewahi kuwa mwanachama wa chama cha  Christian democratic union CDU kinachoongozwa na Kansela Angela Merkel , anasema Mimi binafsi nimempigia kura Obama ili aendelee na wadhifa wake, ana hadhi na anaonekana kuwa mtu mkweli, ningeunga mkono kama wamarekani wangekubali kuwapatia maraisi muhula wa tatu, ila kama Trump akichaguliwa hatutaki hata muhula mmoja, nje hakubaliki na hapendwi kama anavyoonekana na kuongea, na katika eneo la kusini Magharbi mwa Ujerumani tungeweza kusema huyu ni mkulima halisi.

Clinton anaonekana kuwa ni mtu wa kuaminika na anataka kusaidia watu, bila shaka anaonekana kama ni mtu wa Social democratic hapa Ujerumani, nadhani anaweza kufanya kile ambacho anasema atafanya.Nadhani jambo la muhimu zaidi ni kuwa watu wawe na bima ya afya, na Trump anataka kuondoa hilo sio?

Marekani ni taifa la kikristo, na mimi kama Mkristo siwezi kukata tamaa kwa nchi yangu kwa watu wengine, sijui kama Trump ni muumini wa dhehebu lolote, lakini hakuna namna watu wanaweza kumpigia kura Trump, najiuliza hivi hawa watu wanaomuunga mkono na wengine ni watu makini tu wanaweza kuwa wamemuinua hadi mahali fulani.

Ningependa kuwashauri wapiga kura wa Marekani wampigie kura yule ambaye ni afadhali kati ya mashetani hao wawili, hakuna mtu ambaye amekamilika katika dunia, lakini mtu ambaye hana haiba, hachoki kupiga makelele na kujichanganya katika kauli zake mwisho wa siku huwezi kuwa na uhakika utapata kitu gani.

Helmut Kopp mwenye umri wa miaka 46 wa shirika la ushauri wa kiuchumi  anasema Ninafuatilia uchaguzi kwa ukaribu sana kiasi cha kufuatilia mdahalo wa kwanza saa tisa usiku, nilivutiwa lakini kulikuwa na suala la kejeli , sijui niliwekeje suala hili lakini nimeliona kama ni utani kwa kiasi fulani, unaweza kuona kuwa Trump hakuwa amejiandaa na aliendelea kurudia tu taarifa zake, alikuwa na maelezo mengi bila kuwa na majibu ya jinsi gani anataka vitu vifanyike.

USA Donald Trump Wahlkampf North Carolina (picture-alliance/AP Photo/J. Bazemore)

Mgombea urais wa Republican Donald Trump

Wengine wasema wagombea wote wawili ni wazee sana

Mimi sio mshabiki wa Hilary Clinton, nadhani inasikitisha kuona watu milion 320 wanauchaguzi kati ya mzee aliyedhoofu na mwanamke wa miaka 72, wote wawili walipaswa kuwa wanajiandaa na miaka yao ya mwisho na sio kwenda huku na kule kujifanya ni watu wa miaka 50, ambao bado wanafanya kazi na kulipwa vizuri. Ni mjadala ule ule tulikuwa nao kwa John Mc Cain aliyekuwa akigombea pamoja na Obama mwaka 2008 na sasa yeye ni mdogo kwa miaka miwili, ukilinganisha na wagombea wa hivi sasa.

Mfanyabiashara ambaye anafikiri katika mgawanyo, Trump amekuwa akiwakandamiza wafanyakazi wake,najiuliza hivi huyu ni mfanyabiashara wa aina gani. Katika kampuni yetu nadhani tuna watu kutoka karibu mataifa 35 na ninaona hiyo kama ni faida, inawezekanaje mfanyabiashara anyanyase watu kiasi hicho? katika mawazo yangu huo ni ukichaa.

Stefan Hauser mwenye miaka 46 anayefanya kazi katika duka la kimtandao anasema,Trump ana umri wa miaka 70 swali ni je mtu katika umri huo anakuwa na uwezo unaomaanisha kubonyeza alama nyekundu kwa nyuklia? huyu ni babu anayependwa na watu japo ni mtu mwenye akili sana, Clinton bila shaka anataka kuweka rekodi ya kuwa rais wa kwanza mwanamke na kuwa ni miongozi wa ndoa chache ambazo wanandoa wote wawili wamewahi kushika wadhifa huo. Anaitaka hiyo kazi kwa nguvu zote, kwa nini?

Mwandishi: Celina Mwakabwale/dw English

Mhariri:Yusuf Saumu

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com