1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahamiaji 200 haramu wakamatwa Brussels

19 Oktoba 2008
https://p.dw.com/p/Fd0c

Brussels:

Maafisa nchini Ubeligiji wanasema wamewakamata watu 18 baada ya polisi kulivamia kundi la watu wanaodaiwa kuwaingiza watu nchini kimagendo.Tim De Wolf kurtoaka ofisi ya mwendesha mashtaka wa serikali alisema katika hatua hiyo ya Polisi wamewagundua wahamiaji haramu 200 kwenye nyumba kadhaa za mji wa Brussels, wengi wakiwa vijana wa kihindi waliokua waingizwe Uingereza kimagendo. Miongoni mwao ni raia 50 wa India waliojificha katika hekalu la Singasinga katika kitongoji cha Vilvorde. Afisa huyo amesema operesheni hiyo ya leo imelenga katika kulivunja kundi hilo ambalo limekua likiwaingiza Uingereza raia wa India kimagendo kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.