1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wagombea 15 Senegal wataka kura kabla ya rais kuondoka

19 Februari 2024

Wagombea 15 kati ya 20 walioidhinishwa kugombea katika uchaguzi wa urais nchini Senegal, wametaka uchaguzi huo uliocheleshwa ufanyike kabla ya tarehe 2 Aprili, siku ya mwisho ya muhula wa Raid Macky Sall.

https://p.dw.com/p/4caRl
Dakar, Senegal | wafuasi wa kisiasa
Waandamanaji na wafuasi wa kisiasa wanaoshinikiza kuendelea kwa zoezi la kidemokrasia SenegalPicha: John Wessels/AFP

Wagombea 15 kati ya 20 walioidhinishwa kugombea katika uchaguzi wa urais nchini Senegal, wametaka uchaguzi huo uliocheleshwa ufanyike kabla ya tarehe 2 Aprili, ikiwa pia ndio siku ambayo Rais Macky Sall atakamilisha muhula wake madarakani.

Taarifa ya kuahirishwa uchaguzi uliotakiwa kufanyika Februari 25, ilitangazwa masaa machache kabla ya kuanza rasmi kwa kampeni za wagombea. Hatua hiyo iliitumbukiza Senegal katika machafuko mabaya zaidi ya kisiasa kuwahi kushuhudiwa kwa miongo kadhaa.

Soma pia:Upinzani Senegal waongeza shinikizo Macky Sall

Wiki iliyopita, Mahakama Kuu ya Katiba ilibatilisha uamuzi wa kucheleshwa kwa uchaguzi huo. Wagombea hao wamesema inasikitisha kuona kwamba tangu uamuzi wa Baraza hilo la Katiba, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na mamlaka. Hata hivyo, bado kuna utata juu ya tarehe rasmi ya uchaguzi na pia orodha ya wagombea.