WADA yapendekeza Urusi kupigwa marufuku katika IAAF | Michezo | DW | 09.11.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

WADA yapendekeza Urusi kupigwa marufuku katika IAAF

Ripoti ya uchunguzi wa jopo huru kuhusu madai ya matumizi ya dawa za kusisimua misuli miongoni mwa wanariadha imependekeza kuwa Urusi izuiwe kushiriki michezo ya IAAF

mebainika kuwa kiwango cha ufisadi unaohusishwa na matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku katika mchezo huo ni kikubwa mno kuliko kashfa za kifedha zinazolikumba shirikisho la kandanda duniani- FIFA.

Tume huru iliyoundwa na Shirika la Kimataifa la Kupambana na dawa zilizopigwa marufuku michezoni - WADA imetangaza leo matokeo ya uchunguzi wake.

Na miongoni mwa mapendekezo mengi iliyoorodhesha ni kusitishwa uwanachama wa Urusi katika IAAF na wanariadha wake wapigwe marufuku kushiriki katika mashindano yote hadi pale nchi hiyo itasafisha maovu yake ya kukithiri matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini.

Ripoti hiyo inapendekeza kuwa WADA iitangaze maramoja Urusi kuwa mwanachama asiyetekeleza sheria za kupambana na uovu huo na IAAF iipige marufuku katika riadha. Hii ina maana uamuzi kama huo huenda ukawazuia wanariadha wa Urusi kushiriki katika michezo ya mwaka ujao ya Olimpiki mjini Rio de Janeiro

Wakati hayo yakijiri, tume ya maadili ya Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki – IOC imependekeza kuwa aliyekuwa rais wa shirikisho la riadha la kimataifa – IAAF Lamine Diack avuliwe kwa muda uwanachama wa heshima katika kamati hiyo.

Shirikisho la Riadha Ulimwenguni - IAAF limewafungulia maafisa wanne mashtaka ya ukiukaji maadili kwa kuficha matokeo ya vipimo vya utumiaji dawa zilizopigwa marufuku michezoni vinavyomhusisha mwanariadha mmoja wa Urusi. Rais wa zamani wa IAAF Lamine Diack pia anachunguzwa.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP/Reuters
Mhariri: Yusuf Saumu

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com