1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wabunge wa Pakistan wamchagua Shehbaz kuwa waziri mkuu

4 Machi 2024

Wabunge wa Pakistan wamemchagua Shehbaz Sharif kuwa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo kwa mara ya pili.

https://p.dw.com/p/4d8QR
Uchaguzi Pakistan | Shehbaz Sharif
Bunge la Pakistan limemchagua Shebhaz Sharif kuwa waziri mkuu kwa mara ya piliPicha: Ahmad Kamal/Xinhua/IMAGO

Wabunge wa Pakistan wamemchagua Shehbaz Sharif kuwa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo kwa mara ya pili, wiki kadhaa baada ya kufanyika uchaguzi mkuu ambao baadhi ya wanasiasa wamesema ulikumbwa na hitilafu.

Sharif alimshinda mwanasiasa anayeungwa mkono na waziri mkuu wa zamani, Imran Khan, anayetumikia kifungo jela. Shehbaz Sharifi alipata kura 201 wakati mpinzani wake, Omar Ayub, alipata kura 92. Katika uchaguzi mkuu, chama cha Sharif cha PML-N kilishika nafasi ya pili.

Wagombea huru walioungwa mkono na chama cha Imran Khan, PTI, ndiyo waliopata kura nyingi katika uchaguzi huo uliozongwa na madai juu ya udanganyifu.