Vituo 3 vya Olimpik vyafunguliwa | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 08.07.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Vituo 3 vya Olimpik vyafunguliwa

Vituo 3 vya Olimpik kwa waandishi habari vimefunguliwa leo.

Michezo ya olimpik ya Beijing ikikaribia mwezi ujao August 8,waandazi wa michezo hiyo walifungua leo vituo 3 vya kuwahudumia waandishi habari za michez. Ronaldinho amechaguliwa kuichezea Brazil katika dimba la olimpik huko Beijing na Christiano Ronaldo,mshambulizi wa Manchester United hataweza kuichezea Manchestermsimu ukianza kutokana na kufanyiwa matibabu.

Dimba la olimpik:

Rinaldinho,stadi wa Brazil asiewika sana wakati huu, amechaguliwa katika kikosi cha Brazil kwa michezo ijayo ya olimpik ya Beijing, kama mchezaji mmoja kati ya 3 walio vuka umri wa miaka 23.

Mwengine aliechaguliwa katika timu ya Brazil ni Robinho anaeichezea Real Madrid.Kocha Dunga alitangaza kikosi chake .

Wachezaji wasiovuka umri uliowekwa wanajumuisha mchezaji wa kiungo wa Liverpool,Lucas,Anderson wa Manchester United,Diego wa Werder Bremen Alexandre Pato wa AC Milan na Jo,aliejiunga hivi punde na Manchester City.

Brazil, mabingwa wa dunia mara 5, hawakuwahi kutawazwa mabingwa wa dimba wa Olimpik.

Nigeria na Kamerun,zimeshavaa taji hilo kati ya timu za Afrika.Mara hii simba wa nyika watakuwa pia uwanjani na wenzao porini Tembo wa Ivory Coast.

Stadi wa Manchester United, Crsitiano Ronaldo ameumia na amefanyiwsa opresheni nchini Holland.Hivyo, hataweza kuichezea Manchester msimu mpya ukianza.

Daktari wake Niek van Dijk amesema itachukua mwezi kabla yeye kuweza kukisia lini chipukizi huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 23 aweza kucheza tena dimba.

Bingwa mpya wa Tennis wa Wimbledon, Rafael Nadal wa spain,amejitoa kutoka mashindano ya ATP mjini Stuttgart,kusini mwa Ujerumani.Aliarifu hii ni kutokana na kuumia goti.

Nadal aliuwambia mkutano na waandishi habari mjini Stuttgart jana kwamba anahitaji kwanza kupumzika baada ya kucheza miezi 4-5 bila ya kupumua.

Nadal, mwenye umri wa miaka 22 alimshinda bingwa mara 5 wa Wimbledon,mswisi Roger Federer juzi jumapili na kuipatia Spain taji lake jengine baada ya lile la kombe la ulaya la dimba.

Kujitoa kwa Nadal katika mashindano ya Stuttgart,Ujerumani ya ATP yenye zawadi ya kitita cha dala 568,000 ni pigo kwa mashindano hayo.

Mwezi kutoka sasa,michezo ya Olimpik ya Beijing itafunguliwa hapo August 8.Leo waandazi wa michezo hiyo walifungua vituo vitatu vya kuwahudumia waandishi habari na kuahidi kwa chombo chochote cha habari kitakuwa huru kuripoti kutoka pembe yoyote ya jiji la Beijing bila pingamizi.Isitioshe, kutakuwa na uhuru kamili wa mtandao.

kufunguliwa leo kwa Kituo kikuu cha waandishi habari na wapigapicha waliosajiliwa kwa Olimpik na kituo kingine kwa waandishi wasiosajiliwa kumewaruhusu waandishi wachache kati ya wote 25.000 wanaotazamiwa kuanza kazi.Waandishi habari wengine 16.000 watafanya shughuli zao katika kituo kikuu cha radio na TV.

Mbio za baiskeli za Tour De France jana zilikosha nyoyo za wafaransa, baada ya mfaransa, Samuel Dumoulin kushinda hatua ya 3 ya mbio hizi za 2008 na mfaransa mwengine Roman Feillu alivaa jazi ya manjano ya kiongozi wa mbio hizo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com