1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Korea mbili wafanya mkutano wa kilele

Admin.WagnerD18 Septemba 2018

Viongozi wa Korea mbili wamekutana mjini Pyongyang, Korea Kaskazini na kujadiliana kuhusu kuondoa silaha za nyuklia kwenye rasi ya Korea na masuala mengine ambayo yamekuwa kiini cha mzozo baina yao.

https://p.dw.com/p/354Vu
Nordkorea Moon trifft zu drittem Korea-Gipfel in Pjöngjang ein
Picha: Reuters/Pyeongyang Press Corps

Rais Moon Jae-in wa Korea kusini aliwasili Pyongyang kwa mkutano huo wa tatu kwa mwaka huu na Kiongozi wa  Korea kaskazini Kim Jong un. 

Kabla ya kuanza kwa mkutano wao wa kilele rais wa korea kusini  moon jae in na mwenzake wa kaskazini kim juong un walitumia gari la pamoja kukatisha katikati ya mji mkuu wa korea kaskazini Pyongyang ambapo maelfu ya raia waliojipanga barabarani waliwashangalia  wakisema ‘Muungano wa taifa' na kupeperusha bendera za korea zote mbili, wakiashiria  haja ya kuungana tena korea hizo mbili.

Nchini korea kusini lakini mkutano huo umeandamwa na maadamano ya wananchi wanaopinga ushirikiano wa karibu na Korea kaskazini.

Moon ambaye aliwasili Pyongyang siku ya jumanne alilakiwa kwa gwaride la kijeshi na heshima ya zulia jekundu mbele ya mwenyeji wake Kim Jong Un ambaye uwepo wake katika uwanja wa ndege umetajwa na vyombo vya habari kuwa jambo la kushangaza.

Viongozi hao wakiwa wameambatana na wake zao walikumbatiana kwa furaha katika tukio ambalo lilirushwa moja kwa moja katika televisheni nchini Korea Kaskazini na Kusini.

Nuklia bado ni ajenda muhimu

Nordkorea Kim Jong Un trifft Moon Jae-in am Flughafen in Pjöngjang
Picha: picture-alliance/AP Photo/Korea Broadcasting System

Shirika la habari la korea kaskazini limesema likinukuu matamshi ya viongozi waandamizi nchini humo kuwa mkutano huo unatoa nafasi ya kuharakisha ushirikiano wa kimaendeleo baina ya korea mbili ambayo yatatengeneza historia mpya.

Moon, ambaye alifanya juhudi za kuwa mpatanishi katika mazungumzo kuhusu silaha za nuklia kati ya Washington na Pyongyang alisema jana kuwa atatafuta suluhu ya kudumu wakati wa mkutano huo wa siku tatu.

Moon analenga kufanya hadi raundi mbili za mazungumzo kujaribu kumshawishi kiongozi wa Korea kaskazini kuchukua hatua kamili kuelekea kuikongoa mifumo ya silaha za nuklia na makubaliano yoyote yale yatayawasilisha wakati wa mkutano wake na Rais Donald trump wa Marekani watapokutana mjini New York pembezoni mwa mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa baadae mwezi huu.

Marekani inataka mpango kamili kuondoa nuklia

Südkorea Moon Jae-in und Kim Jong Un in einer Fernsehübertragung in Seoul
Picha: picture-alliance/AP Photo/Ahn Young-joon

Kim jong un alitangaza azma yake ya kuondoa silaha za nuklia kwenye rasi ya korea maema mwezi aprili na mei na pia wakati wa mkutano wake wa kihistoria na rais wa marekani Donald Trump nchini Singapore mwezi june mwaka huu.

Hata hivyo matamshi yake hayakutoa maelezo kamili ya ni linin a kwa namna gani mpango huo utakamilika na hivi sasa majadiliano kati ya Pyongyang na Washington yamesusua.

Marekani imesema inataka mpango kamili wa wa kuondoa silaha za nuklia kwenye eneo hilo.

Rais Donald Trump wa Marekani mwezi  uliopita aliifuta ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo iliyopangwa nchini korea kaskazini akisema hakuna hatua ya kuridhishwa iliyopigwa kuelekea kuondoa silaha za nuklia kwenye rasi ya Korea.,

Ziara hiyo ya moon ni ya kwanza kufanywa na kiongozi wa korea kusini nchini korea kaskazini katika kipindi cha miaka 11 iliyopita baada ya rais Roh Moo-hyun wa Korea Kusini kuizuru Korea Kaskazini  2007.

Mwandishi: Rashid Chilumba/AFP/AP

Mhariri. Mohammed Abdul-Rahman