1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa dunia waadhimisha miaka 75 ya kuundwa UN

Sekione Kitojo
22 Septemba 2020

Viongozi wa dunia waliungana pamoja (21.09.2020) kwa njia ya vidio kuadhimisha  miaka 75 tangu pale Umoja wa mataifa ulipoasisiwa. Kansela wa Ujerumani Angela  Merkel amesema taasisi hiyo inahitaji umoja zaidi.

https://p.dw.com/p/3ipkQ
USA, New York I 75. Jahrestag der Vereinten Nationen
Picha: Manuel Elías/United Nations/dpa/picture-alliance

Katika tukio  la  Umoja  wa  Mataifa  kufikisha  miaka 75  tangu kuundwa, kansela  wa  Ujerumani  Angela  Merkel  jana  alitoa wito wa mageuzi katika  taasisi  hiyo  ya  kimataifa pamoja na  umoja mkubwa  zaidi  baina ya  wanachama  wake.

Mwishoni Umoja  wa  Mataifa  unaweza  kuwa   kituo  kizuri  tu iwapo wanachama  wake  watakuwa  na  umoja," Merkel  alisema katika  ujumbe  wa  vidio  aliotoa jana jioni  katika  sherehe  za kuadhimisha  miaka  75  tangu  kuundwa  kwa  Umoja  wa  Mtaifa.

Deutschland Libyen-Konferenz in Berlin
Kansela Angela Merkel(kulia) akiwa pamoja na katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres (kushoto)Picha: AFP/M. Kappeler

"Wale wanaoamini  kwamba  wanaweza  kufanya vitu vyao vizuri zaidi peke  yao wanakosea. Mfano uliopo ni janga  la  COVID-19 ambalo limeonesha kwamba  matatizo ya dunia  yanahitaji uelewa na  ushirikiano kupindukia mipaka ya nchi  katika kila eneo. Mwishoni mwa  siku, Umoja wa  Mataifa  unaweza  kufanya kazi  vizuri  zaidi iwapo wanachama  wake watakuwa  na  Umoja."

Kansela  amesemaMara  nyingi  baraza  la  Usalama  la  Umoja  wa Mataifa  linakwama  wakati  uamuzi  wa  wazi  unahitajika," akilizungumzia  tawi  hilo  la  Umoja  wa Mataifa  lenye jukumu  la kuhakikisha  kuwa  amani  ya  kimataifa  na  usalama inapatikana. "Tunahitaji  mageuzi."

Maslahi binafsi

Merkel pia alisema maslahi  binafsi  ya  wanachama  mmoja  mmoja mara  nyingi   yanasababisha  shirika  hilo kushindwa  kufanikisha malengo  yake.

Naye  katibu  mkuu  wa  Umoja  wa  mataifa  Antonio Guterres ametoa  wito wa  kurejeshwa  hali  ya muungano  zaidi, ambao ni msingi  Umoja  wa  Mataifa. Wito  huo  umerudiwa  na  viongozi kubwa  na  ndogo , masikini  na  tajiri  duniani  kote.

USA, New York I 75. Jahrestag der Vereinten Nationen
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio GuterresPicha: Eskinder Debebe/UN Photo/Imago Images

Lakini  licha ya  kuwapo  hotuba  za  kutia  moyo , ni  dhahiri kwamba changamoto  bado  ziko katika  kuungana  na kupambana  na  janga la  virusi vya corona, pamoja  na  mizozo  kadhaa  midogo  kuanzia mashariki  ya  kati  hadi  Afrika, na  kufikia  malengo  ya  Umoja  wa mataifa  ya  kufuta  umasikini  uliokithiri na kulinda  mazingira na kufikia  lengo  lililowekwa la  mwaka 2030.

Mijadala ya  kila  mwaka  ya  baraza  kuu  la  Umoja  wa  mataifa inaanza  rasmi  leo, ambapo  viongozi  wa  dunia  watatoa  hotuba zao  kupitia  vidio  badala  ya  kukusanyika  mjini  New York. Hii  ni mara  ya  kwanza  kufanyika  hivyo  kutokana  na  janga  la  virusi vya  corona.