Vikosi vya Iraq kusimamia Basra | Habari za Ulimwengu | DW | 10.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Vikosi vya Iraq kusimamia Basra

BAGHDAD

Waziri Mkuu was Uingereza Gordon Brown ametangaza wakati wa ziara yake ya ghafla mjini Basra nchini Iraq kwamba vikosi vya Iraq vitachukuwa udhibiti wa kusimamia mji huo katika kipindi kisichozidi wiki mbili katika jimbo hilo la kusini ambapo vikosi vya Uingereza vimewekwa.

Brown ambaye amewasili Basra jana jioni ameviambia vikosi vya Uingereza kwamba umwagaji damu haukukomeshwa nchini humo lakini Iraq hivi sasa iko katika nafasi nzuri kuliko ilivyokuwa kabla.

Waziri Mkuu huyo wa Uingereza anatazamiwa kuwa na mazungumzo kwa njia ya simu na Waziri Mkuu wa Iraq Nuri al Maliki na Waziri wa Ulinzi Abdel Qadir al Ubaydi.

Wakati huo huo mjini Baghdad mizinga imeshambulia gereza la wizara ya mambo ya ndani hapo jana na kuuwa takriban wafungwa saba na kujeruhi wengine 23.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com