Vietnam yakamata nusu tani ya pembe za ndovu | Matukio ya Afrika | DW | 02.12.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

PEMBE ZA NDOVU

Vietnam yakamata nusu tani ya pembe za ndovu

Maafisa wa forodha nchini Vietnam wamekamata kilo 529 za pembe za ndovu zilizokuwa zimefichwa katika shehena ya mbao kutoka Nigeria, na hivyo kuifanya ya pembe zilizokamatwa wiki hii kuwa tani nzima.

Afisa wa forodha katika mji wa Ho Chi Minh, Pham Quang Nam, ameliambia shirika la habari la Ujerumani (dpa) kwamba maafisa walipewa taarifa kutoka duru za kimataifa kabla ya kuwakamata wahalifu hao.

Walanguzi wa biashara ya pembe za ndovu mara nyingi huficha pembe katikati ya mbao, lakini matumizi ya kifaa maluum cha ukaguzi wa mbao kinawasaidia maafisa wa forodha kuzikamata pembe hizo.

Walanguzi hao hutumia sana nchi ya Vietnam kama kituo cha kupitishia mzigo wao unaokwendea China.