1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGabon

Gabon: Utawala wa kijeshi wamemteua Waziri Mkuu wa mpito

8 Septemba 2023

Utawala wa kijeshi nchini Gabon umemteua kiongozi wa zamani wa upinzani, Raymond Ndong Sima, kuwa waziri mkuu wa serikali ya mpito.

https://p.dw.com/p/4W6l6
Raymond Ndong Sima
Picha: Scott Ngokila/Afrikimages Agency/IMAGO

Uteuzi huo ulifanyika hapo jana Alhamisi na ulitangazwa kwenye televisheni ya taifa. Sima, mwanauchumi mwenye umri wa miaka 68, alikuwa mkosoaji mkubwa wa Rais Ali Bongo aliyeondolewa madarakani na maafisa wa kijeshi mnamo Agosti 30.

Aliwahi kuwa  waziri mkuu wa Bongo  kuanzia mwaka 2012 hadi mwaka 2014. Alijiuzulu mwaka 2014 na kugombea urais 2016 na kwa mara nyingine tena mwaka huu chama chake kilikuwa sehemu ya muungano wa upinzani.

 Kiongozi wa kijeshi wa Gabon jenerali Brice Oligui Nguema ameahidi kuleta mageuzi ya kiuchumi na amesema ataandaa uchaguzi huru na wa haki, ingawa hajasema ni lini uchaguzi huo utafanyika.