Urusi yaanza vizuri kombe la mabara | Michezo | DW | 18.06.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Urusi yaanza vizuri kombe la mabara

Urusi mwenyeji  wa   kombe la  mabara  imeanza  vizuri  jana  baada  ya  kuishinda  New Zealand  kwa  mabao 2-0.

Wachezaji  wa  Urusi  ambao wengine  hata  hawafahamiki  nje ya nchi  yao  walilazimisha  bao  la  kwanza  lililofungwa  na  mchezaji  wa  New Zealand Michael Boxal  katika  dakika  ya  31, na  mshambuliaji Fyodor Smolov  aliongeza  bao la  pili  katika dakika  ya  69.

St Petersburg2017 FIFA Confederations Cup Eröffnung (picture-alliance/Tass/dpa/V. Sharifulin)

Sherehe za ufunguzi wa michuano ya kombe la mabara

Timu  zote zilisimama  uwanjani  wakisikiliza  hotuba  iliyotolewa  na  rais  wa  Urusi  Vladimir Putin  na  rais  wa  shirikisho  na  kandanda  duniani  Gianini Infantino , kabla  ya  kuruhusiwa kukamilisha  maandalizi  ya  pambano  hilo.

Siku  chache  kabla , Putin  aliwataka  wachezaji  wa  timu  hiyo  kupata  matokeo  mazuri  ili kuweza  kuwafurahisha  wananchi  wa  Urusi.

Fußball FIFA Confederations Cup Putin und Infantino (picture-alliance/dpa/D. Astakhov)

Rais wa FIFA Gianini Infantino na rais wa Urusi Vladimir Putin katika michuano ya kombe la mabara mjini St. Petersberg, Urusi

Leo  ni  kati  ya  Ureno  mabingwa  wa  bara  la  Ulaya  dhidi  ya  Mexico.

Mwandishi : Sekione Kitojo / ape