1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi kuwafidia wahanga wa shambulio la kigaidi

Jane Nyingi
13 Aprili 2017

Urusi ametangaza katika kipindi cha miezi mitatu ijayo itakata rufaa kupinga agizo la mahakama ya ulaya  kulipa mamilioni ya Euro kama  fidia kutokana na kushindwa kuzima shambulizi la kigaidi mwaka 2004.

https://p.dw.com/p/2bDOC
Beslan Schauplatz Geiseldrama
Picha: DW/W.Bodrow

Shambulizi hilo lilitokea katika shule moja  kusini mwa mji wa Beslan. Katika taarifa kwa vyombo vya habari wizara ya ulinzi nchini  humo imesema inaamini uamuzi huo wa mahakama ya Ulaya ya haki za binadamu iliko mjini  Strasbourg haukuzingatia taarifa za kweli. Mahakama hiyo imeiagiza Urusi kulipa  karibu Euro millioni 3 (Dola millioni 3.2)kufuatia kesi iliyowasilishwa na raia 409 wa Urusi ambao walionusurika shambulio au  jamaa za waathirika.Mahakama hiyo ya haki za binadamu imesema maafisa wakuu nchini Urusi walikuwa wanafahamu kuhusu mipango ya shambulizi la kigaidi  dhidi ya taasisi ya elimu  katika eneo hilo ,lakini hakuna hatua za kutosha walizochukua kuilinda shule  au kutoa tahadhari. Mahakama iligundua mapungufu chungu nzima kuhusu  jinsi operesheni ya usalama ilivyoendeshwa.Matumizi ya  vifaru, silaha zinazotumiwa kufyetua magurunedi na zana nyingine ulisababisha majeruhi  miongoni mwa mateka.Wanamgambo waliokuwa na silaha nzito kutoka kusini mwa eneo la Caucasus nchini Urusi  waliwakamata  mateka zaidi ya watu 1,100 katika tukio lilochukua saa 50.Tukio hilo  lilifanyika siku ya kwanza ya kufunguliwa shule Septemba mosi mwaka 2004. Zaidi ya watu 330  wakiwemo watoto 180 weliuawa  na mamia ya wengine wakajeruhiwa. Kundi moja lililojitenga la wapiganaji wa kiislam  lilikiri kuhusika katika shambulizi hilo. Kwa miongo kadhaa  kumekuwepo na mashmabulizi  yanayoendeshwa na wanagamabo wa kiislam  huko Caucasus ambako ndiko iliko mji huo wa Beslan.

Russland Russisch-Tschetschenischer Konflikt | 2004 Geiselnahme in Schule von Beslan
Watoto waliojeruhiwa kufuatia shambulizi hiloPicha: picture-alliance/dpa/S. Dolzhenko

Mwandishi:Jane Nyingi/AFP/AP
Mhariri:Yusuf Saumu