1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroKimataifa

UN yatahadharisha tabia ya kutumia mabavu kutatua mizozo

28 Februari 2026

Mkuu wa haki za binaadamu wa Umoja wa Mataifa amesema viongozi wamekuwa wakitumia madaraka vibaya na kutoa kipaumbele kwa matumizi ya nguvu kutatua mizozo, hali inayopelekea kuongezeka kwa idadi ya mizozo kote duniani.

https://p.dw.com/p/59ZpS
Mkuu wa haki za binaadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk
Mkuu wa haki za binaadamu wa Umoja wa Mataifa Volker TurkPicha: DW

Volker Turk ameliambia Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa hapo jana mjini Geneva kuwa kunashuhudiwa "mparaganyiko duniani" kufuatia kitendo cha kuchukulia kawaida matumizi ya nguvu, huku akitolea mifano mizozo ya Sudan, Ukraine na maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu.

Turk amesema idadi ya  migogoro inayohusisha silaha imeongezeka maradufu  tangu mwaka 2010 na kufikia karibu migogoro 60, huku akitamatisha kuwa kwa sasa dunia inazidi kuwa eneo hatari zaidi.