1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yaonya kuhusu IDF kuwataka raia kuondoka Gaza

11 Julai 2024

Umoja wa Mataifa umetoa tahadhari kuhusu usalama wa raia baada ya Jeshi la Israel, IDF kuwataka wakaazi wote wa mji wa Gaza kuondoka, katika kile ambacho waangalizi wanasema ni ishara ya operesheni mpya za kijeshi.

https://p.dw.com/p/4i9hY
Vifaru vya Israel katika mji wa Gaza
Vifaru vya Israel katika mji wa GazaPicha: Jim Hollander/UPI Photo/Newscom/picture alliance

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kiutu, OCHA imeonya katika taarifa yake kuwa maagizo ya Israel kwa watu kuondoka Gaza, yatachochea mateso makubwa kwa familia za Wapalestina, ambao wengi wao wameyakimbia makaazi yao mara nyingi. 

Stéphane Dujarric, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amesema raia hao wanapaswa kulindwa, na mahitaji yao muhimu lazima yatimizwe iwe wanakimbia au wanabakia. 

Soma pia:Jeshi la Israel latoa amri ya watu kuuhama mji wa Gaza

Dujarric amezitaka pande zote zinazohusika katika mzozo huo, kuheshimu sheria za kimataifa za kiutu, kwa wakati wote.