1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiHaiti

Umoja wa Mataifa waonya kuhusu hali mbaya inayoendelea Haiti

23 Aprili 2024

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia watoto UNICEF ameonya kuhusu hali mbaya inayoendelea Haiti kutokana na vurugu za magenge ya wahalifu.

https://p.dw.com/p/4f4So
Haiti- Raia aliyejeruhiwa kwa kupigwa risasi na magenge ya wahalifu
Raia aliyejeruhiwa kwa kupigwa risasi na magenge ya wahalifu katika mji mkuu Port-au-Prince nchini Haiti:19.04.2024Picha: Ramon Espinosa/AP Photo/picture alliance

UNICEF imesema vurugu hizo zinayaweka hatarini maisha ya watoto wapatao 58,000 ambao wanakabiliwa na viwango vya juu vya utapiamlo.

Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Catherine Russell amesema theluthi mbili ya watoto wa Haiti wanahitaji misaada, huku wanawake na wasichana wakilengwa na "viwango vilivyokithiri" vya unyanyasaji wa kijinsia na kingono.

Russell ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa  hali nchini Haiti ni mbaya mno na inazidi kuwa mbaya kila siku, hasa katika mji mkuu wa Port-au-Prince unaodhibitiwa kwa asilimia 90 na magenge hayo, sasa unakaribia kuzingirwa kabisa kutokana na vizuizi vya angani, baharini na nchi kavu.