Migogoro
Ukraine, Qatar, UAE kushirikiana katika sekta ya ulinzi
28 Machi 2026
Matangazo
Qatar na Ukraine zimetia saini makubaliano yanayohusisha ushirikiano katika kupambana na kitisho cha droni na makombora. Kwa upande wa Falme za Kiarabu Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema amekutana na Rais Mohamed bin Zayed Al Nahyan na kwamba wapo kwenye hatua za kukamilisha makubaliano.
Iran yadai kushambulia kituo cha mifumo ya kupambana na droni ya Ukraine nchini UAE
Ameyasema hayo wakati Iran ikiarifu kuwa imekishambulia kituo cha Ukraine chenye mifumo ya kupambana na droni kilicho katika Falme za Kiarabu. Iran inadai kituo hicho kilitumiwa kuvisaidia vikosi vya Marekani kuishambulia. Hata hivyo Ukraine imekanusha taarifa ya kushambuliwa kwa kituo hicho na kusema madai ya Iran ni ya uongo.