1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUgiriki

Ugiriki: Wahamiaji 550,000 wako Libya wakisubiri kuja Ulaya

10 Mei 2026

Ugiriki imetahadharisha kuwa zaidi ya wahamiaji 550,000 wapo nchini Libya wakisubiri fursa ya kusafiri kuelekea barani Ulaya kwa kutumia safari hatari za baharini ambazo zimekuwa zikisababisha vifo vya mamia ya watu.

https://p.dw.com/p/5DY74
Wahamiaji wakiokolewa karibu na pwani ya Ugiriki
Wahamiaji wakiokolewa karibu na pwani ya UgirikiPicha: Marios Lolos/Photoshot/picture alliance

Hayo yameelezwa Jumapili na Waziri wa Uhamiaji wa Ugiriki Thanos Plevris aliyeongeza kuwa serikali mjini Athens kwa ushirikiano na shirika la udhibiti wa mipaka la Umoja wa Ulaya Frontex, pamoja na mamlaka za Libya wameanzisha mkakati wa kupambana na safari hizo na kukabiliana na magenge yanayowasafirisha watu hao kimagendo.

Siku ya Jumapili, walinzi wa pwani wa Ugiriki wamewaokoa wahamiaji 125 waliokuwa katika boti ndogo mbili zilizopatikana pwani ya kusini ya Krete,  huku kukitarajiwa kuwasili kwa boti zingine za wahamiaji kutoka Libya.

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR, mwaka jana, wahamiaji wapatao 42,000 waliwasili katika visiwa vya Ugiriki huku watu 107 wakiripotiwa kufa maji katika bahari ya Mediterania.