1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Ugaidi

Uganda yatangaza kumkamata kamanda wa kundi la ADF

20 Mei 2024

Wakati wa operesheni hiyo, watu tisa wakiwemo watoto pia waliokolewa kutoka eneo la jimbo la Ituri mashariki mwa Kongo.

https://p.dw.com/p/4g4rg
DR Kongo | Vita dhidi ya ADF Beni
Vikosi vya UPDF na FARDC vinashirkiana dhidi ya kundi la ADFPicha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Jeshi la Uganda limesema limemkamata kamanda wa kundi la waasi la ADF linaloshirikiana na kundi linalojiita  dola la kiislamu, ambaye ni mtaalamu wa kutengeneza mabomu yaliyotumiwa na kundi hilo kutekeleza mashambulizi mabaya.

Kamanda huyo Anywari Al-Iraq ambaye ni raia wa Uganda, alikamatwa katika maeneo ya jangwani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kunakopatikana kundi la ADF.

Soma pia: Uganda yapuuza ripoti ya UN kuhusu operesheni yake Kongo

Katika operesheni ya kumsaka kamnda huyo, watu tisa wakiwemo watoto waliokolewa kutoka katika eneo hilo lililopo mkoani Ituri Mashariki mwa DRC, bidhaa nyengine za kutengenezea mabomu pia zilipatikana huko.

Kundi hilo la waasi wa ADF lilianza harakati zake nchini Uganda lakini limekuwa na ngome yake nchini Congo tangu miaka ya 90. Lilitangaza  kushirikiana na kundi linalojiita  dola la kiislamu mwaka 2019 na linatuhumiwa kuwauwa mamia ya wanavijiji katika mashambulizi ya mara kwa mara katika miaka ya hivi karibuni.