Ufaransa itayari kuingilia kati Chad | Habari za Ulimwengu | DW | 06.02.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Ufaransa itayari kuingilia kati Chad

NDJAMENA:

Balozi wa Ufaransa nchini Chad amesema,mji mkuu Ndjamena na maeneo yanayouzunguka mji huo yamedhibitiwa na serikali ya Chad.Wakati huo huo, Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy ameonya,iwapo itaihitajika ataviamuru vikosi vya Ufaransa vilivyo nchini Chad kuchukua hatua ili kuzuia mapigano mapya kati ya vikosi vya serikali na makundi ya waasi.Sarkozy ametamka hayo kufuatia hati iliyoidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ikihalalisha hatua hiyo.

Tangu waasi walipojaribu kuivamia Ikulu mjini Ndjamena hapo siku ya Jumamosi, kiasi ya watu 50,000 wameuhama mji huo-wengi wao wakikimbilia upande wa pili wa mpaka nchini Kamerun.Maafisa wa Chama cha Msalaba Mwekundu nchini Chad wamesema,mamia ya raia wameuawa na takriban 1,000 wengine wamejeruhiwa katika mapambano hayo.Wakati huo huo,kuna shaka iwapo tangazo la kuweka chini silaha linafanya kazi,baada ya maafisa kadhaa wa waasi kutamka kuwa watakubali kuacha mapigano ikiwa tu Rais Idriss Deby atajiuzulu.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com