1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Ufaransa yawahamisha raia wake na wa kigeni

Tatu Karema
27 Machi 2024

Ufaransa imewahamisha zaidi ya raia wake 170 na karibu raia 70 wa mataifa mengine kwa helkopta za jeshi kutoka nchini Haiti ambako kumekumbwa na ghasia.

https://p.dw.com/p/4eBdz
Ghasia za Haiti kati ya vikosi vya usalama na magenge ya wahalifu kwenye mji wa Port-au-Prince
Maafisa wa polisi nchini Haiti wakikabiliana na wahalifu katika mji wa Port-au-Prince, Machi 21,2024. Mataifa a kigeni yameanza kuondoa raia wao kutokana na hofu ya usalamaPicha: Ralph Tedy Erol/REUTERS

Wizara ya Mambo ya Nje a Ufaransa imethibitisha kuhamishwa kwa watu hao, ambao imesema walikuwa kwenye mazingira magumu.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa watu hao walipelekwa hadi kwenye boti la jeshi la wanamaji ambalo litawasafirisha leo kuelekea Fort-de-France, mji mkuu wa kisiwa cha Carribean cha Martinique, kinachomilikiwa na Ufaransa.

Kulingana na taarifa hiyo, takriban raia 1,100 wa Ufaransa wanaishi Haiti, wengi wao wakiwa na uraia pacha.

Ufaransa ilitangaza kuanza kwa safari hizo za ndege siku ya Jumapili na kusema watu wanaotaka kuondoka nchini Haiti wanapaswa kuwasiliana na ubalozi wake mjini Port-au-Prince.

Port-au-Prince imekumbwa na ghasia za magenge ya uhalifu zilizozuka mwishoni mwa mwezi Februari, na kusababisha kujiuzulu kwa waziri mkuu Ariel Henry mapema mwezi huu.