1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRC 'haitapiga mnada' rasilimali za madini kwa Marekani

23 Septemba 2025

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Felix Tshisekedi amesema mkataba wa amani uliosainiwa mwezi Juni kati ya nchi yake na Rwanda na kusimamiwa na Marekani haujasitisha mapigano mashariki mwa Kongo.

https://p.dw.com/p/50vLh
Munich, Ujerumani 2025 | Rais wa Kongo, Felix Tshisekedi
Rais wa Kongo, Felix Tshisekedi amesema hawatouza rasilimali zao za madiniPicha: Michaela Stache/AFP

Akizungumza Jumatatu na waandishi habari mjini New York, Tshisekedi amesema anamshukuru Rais Donald Trump kwa kujaribu kuumaliza mzozo huo.

Amesema licha ya kuunga mkono upatanishi wa Marekani, haimaanishi kuwa watauza rasilimali zao za madini.

Utawala wa Trump umesema una nia ya kumaliza mapigano ambayo yamewaua maelfu ya watu mwaka huu na kuvutia mabilioni ya dola kwa wawekezaji wa mataifa ya Magharibi kuwekeza katika eneo lenye utajiri wa madini ya tantalum, dhahabu, cobalt, shaba na lithium.

Muda wa mwisho wa kutekeleza sehemu ya mpango huo wa Marekani ni mwezi huu.

Wakati huo huo, Spika wa Bunge la Kongo, Vital Kamerhe ametangaza kujiuzulu wadhifa wake.

Kamerhe amechukua uamuzi huo Jumatatu usiku, kabla ya wabunge hawajapiga kura ya kutokuwa na imani naye.