1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Trump aahidi ushuru kwa nchi zinazoshindwa kuzuia wahamiaji

7 Juni 2024

Mgombea wa urais kupitia cha Republican Donald Trump amesema ikiwa atashinda uchaguzi wa mwezi Novemba, huenda akaziwekea ushuru nchi, zinazoshindwa kudhibiti mmiminiko wa wahamiaji wasio na vibali wanaoingia Marekani.

https://p.dw.com/p/4gl0Q
Marekani | Mgombea Urais kupitia Republican, Donald Trump
Donald Trump anayegombea urais kupitia chama cha Republican nchini Marekani asema atatumia ushuru kama njia ya kuyaadhibu mataifa yanayoshindwa kuzuia wahamiaji haramau wanaoingfia MarekaniPicha: Spencer Platt/Getty Images

Trump amesema siku ya Alhamisi kwamba nchi atakazoziwekea ushuru ni pamoja na China.

Trump ametoa matamshi hayo akiwa katika jimbo la Arizona alipokuwa akijibu maswali ya wakaazi wa eneo hilo, ingawa hakufafanua ukubwa wa ushuru atakaouanzisha.

Alipoulizwa kuhusu njia atakazotumia kudhibiti mmiminiko huo wa wahamiaji wanaoingia kinyume cha sheria nchini humo, Trump alisema tu kwamba Marekani ina nguvu kubwa kiuchumi na kuongeza kuwa ikiwa nchi kama China haisaidii kudhibiti wahamiaji wanaoingia Marekani, basi atatumia njia kama hiyo ya ushuru.

Usalama wa mpakani umekuwa ajenda muhimu kwa Wamarekani katika uchaguzi utakaofanyika Novemba 5, na kuwakutanisha Trump na Rais Joe Biden.