1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania yafuzu fainali ya michuano ya AFCON

Sylvia Mwehozi
8 Septemba 2023

Timu ya taifa ya kandanda ya Tanzania Taifa Stars ni miongoni mwa timu zilizofuzu kucheza fainali ya mashindano ya kombe la Afrika AFCON baada ya kutoka sare na Algeria.

https://p.dw.com/p/4W5jS
Tanzania kandanda
Kikosi cha Taifa Stars 2021Picha: Ericky Boniphase

Timu ya taifa ya kandanda ya Tanzania Taifa Stars ni miongoni mwa timu zilizofuzu kucheza fainali ya mashindano ya kombe la Afrika AFCON baada ya kutoka sare na Algeria. Ghana na Angola nazo zimefanikiwa kusonga mbele baada ya kumaliza nafasi ya kwanza na ya pili katika kundi E.

Kenya na Tanzania zaangukia pua

Taifa Stars imemaliza nafasi ya pili katika kundi F ikiwa na alama 8 na Algeria wakiongoza kundi hilo kwa alama 16. Uganda ambao walikuwa kundi moja na Taifa Stars wameshindwa kufuzu baada ya kukosa pointi moja licha ya kuifunga Niger mabao 2-0 na hivyo kuondoka na alama 7. 

Jumla ya timu 24 zitashiriki michuano ya AFCON itakayofanyika nchini Ivory Coast mwanzoni mwa mwaka ujao.