1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania, Rwanda, Zimbabwe zarejesha dawa ya kikohozi ya J&J

John Juma
16 Aprili 2024

Wadhibiti wa dawa nchini Tanzania, Rwanda na Zimbabwe wameamuru kusitishwa kwa matumizi ya dawa ya kikohozi kwa watoto iliyotengenezwa na kampuni ya Johnson & Johnson kama hatua ya tahadhari.

https://p.dw.com/p/4eqSg
Afya | Dawa ya kikohozi kwa watoto
Dawa ya kikohozi kwa watotoPicha: Lev Dolgachov/Zoonar/picture alliance

Hii ni baada ya mamlaka za Nigeria kusema kuwa vipimo vya maabara vilikuta viwango vikubwa vya sumu. Nchi hizo zinaungana na Nigeria, Kenya na Afrika Kusini katika kusitisha matumizi na kuamuru kurejeshwa dawa hiyo, ambayo inatumika kutibu kikohozi na homa kwa watoto. 

Mamlaka ya Dawa na Vifaa vya Matibabu nchini Tanzania - TMDA imesema imeanza kurejesha dawa hiyo Aprili 12 baada ya kusikia matokeo ya vipimo vya Nigeria.

Soma pia:Kenya yarejesha dawa ya kikohozi ya watoto kutoka kampuni ya J&J

Msemaji wa TMDA, Gaudensia Simwanza amesema hilo ni zoezi lisilohusisha uchunguzi bali ufuatiliaji ili kuhakikisha kuwa dawa zilizoathirika zinaondolewa sokoni. 

Msemaji ya kusimamia usalama wa dawa nchini Kenya amesema matokeo ya vipimo vyake kuhusu dawa hiyo ya maji maji itakuwa tayari Jumatano.