1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Taiwan yashtumu tabia ya ''uchochezi wa kijeshi'' ya China

23 Mei 2024

Taiwan imesema leo kwamba inasikitisha kuona kuwa China imeanzisha luteka za kijeshi karibu na kisiwa hicho kinachojitawala siku chache baada ya Lai Ching-te kutawazwa kama kiongozi mpya wa eneo hilo.

https://p.dw.com/p/4gC59
Rais wa Taiwan Lai Ching-te akielezwa namnya ya kurusha roketi
Rais wa Taiwan Lai Ching-te akielezwa namnya ya kurusha roketiPicha: Ann Wang/REUTERS

Taiwan imesema leo kwamba inasikitisha kuona kuwa China imeanzisha luteka za kijeshi karibu na kisiwa hicho kinachojitawala siku chache baada ya Lai Ching-te kutawazwa kama kiongozi mpya wa eneo hilo.

Katika taarifa, msemaji wa ofisi ya rais, Karen Kuo, amesema inasikitisha kuona China ikitumia tabia za kijeshi za uchochezi na za pande moja zinazotishia demokrasia na uhuru wa Taiwan pamoja na amani na utulivu wa kikanda.

Soma pia: Lai Ching-te aapishwa rasmi kuwa rais mpya wa Taiwan 

Kuo ameongeza kusema wakati kisiwa hicho kinachojitawala kinapokabiliwa na vitisho na changamoto kutoka nje, kitaendelea kutetea demokrasia yake.

Wakati huo huo, Rais wa Taiwan Lai Ching-te amesema kuwa atasimama katika mstari wa mbele wa vita pamoja na wanajeshi wa nchi hiyo kulinda usalama wa kitaifa wa Taiwan bila ya kutaja moja kwa moja luteka hizo za kijeshi za China.