1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Taiwan yasema "vitimbi" vya jeshi la China vimeongezeka

15 Mei 2024

Maafisa wa serikali ya Taiwan wamesema katika wiki za karibuni jeshi la China limetuma meli na kurusha ndege za kivita karibu zaidi na kisiwa hicho kuliko lilivyowahi kufanya hapo kabla.

https://p.dw.com/p/4fs92
Taiwan |China
Meli ya walinzi wa pwani ya China ikiipita meli kama hiyo ya TaiwanPicha: TAIWAN COAST GUARD/AFP

Maafisa wa serikali ya Taiwan wamesema katika wiki za karibuni jeshi la China limetuma meli na kurusha ndege za kivita karibu zaidi na kisiwa hicho kuliko lilivyowahi kufanya hapo kabla.

Maelezo yao yanarandana na ripoti zinazokusanywa na serikali ya Taiwan ambazo zinaonesha tangu mwishoni mwa mwezi Aprili idadi kubwa zaidi ya meli na ndege za China zimefanya luteka karibu kabisa kisiwa hicho. Sehemu ya luteka hizo inajumuisha mazoezi ya mfano ya kuivamia Taiwan kutokea China bara.

Je, mzozo wa China na Taiwan kuongezeka baada ya uchaguzi?

Maenesho hayo ya nguvu za kijeshi za China yanashuhudiwa katika wakati Taiwan inajiandaa kumwapisha rais mpya Lai Ching-te mnamo Jumatatu inayokuja. Taiwan imesema ilitarajia kuona vitendo vya namna hiyo vinaongezeaka kutoka Beijing ambayo inakizingatia kisiwa hicho chenye utawala wake wa ndani kuwa sehemu ya himaya ya China.