1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTaiwan

Taiwan yaripoti shughuli zaidi ya kijeshi za China

Tatu Karema
23 Desemba 2023

Taiwan imeripoti kuwepo kwa ndege na meli za kivita za China, zinazozunguka kisiwa hicho leo ikiwa ni pamoja na ndege kuvuka mstari wa kati katika mlango wa bahari wa Taiwan wakati China ikiendeleza shughuli za kijeshi

https://p.dw.com/p/4aWx6
Ndege za kivita za China aina ya J-11B wakati wa mazoezi ya kuadhimisha miaka 70 tangu kukamilika kwa vita ya pili ya dunia mnao Julai 2, 2015
Ndege za kivita za ChinaPicha: Jason Lee/REUTERS

Wizara ya ulinzi ya Taiwan imesema tangu mwendo wa mchana wa leo kwa saa za eneo hilo, iligundua ndege za kivita za China aina ya J-10, J-11 na J-16 katika anga ya maeneo ya Kaskazini, Kati na Kusini Magharibi mwa kisiwa hicho kinachojitawala.

Mstari huo wa kati, wakati mmoja ulitumika kama kizuizi kisicho rasmi kati ya pande hizo mbili lakini ndege za China sasa huruka mara kwa mara juu yake.

Soma pia.Taiwan yaionya China kwa kurusha ndege za kivita

Wizara hiyo ya ulinzi pia imesema kuwa imetuma vikosi vyake kufuatilia matukio hayo.

China haijatoa tamko lolote kuhusu mfululizo wa shughuli zake za kijeshi za hivi karibuni

karibu na Taiwan.