1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroChina

Taiwan yaionya China kwa kurusha ndege za kivita

18 Septemba 2023

Baada ya zaidi ya ndege 100 za kivita na meli tisa za jeshi la wanamaji za China kuripotiwa katika maeneo yaliyo karibu na kisiwa hicho kinachojitawala.

https://p.dw.com/p/4WSdu
Taiwan yaionya China kwa kurusha ndege 103  za kivita karibu na eneo lake
Taiwan yaionya China kwa kurusha ndege 103 za kivita karibu na eneo lakePicha: EASTERN THEATRE COMMAND/REUTERS

Taiwan imetoa wito kwa China hivi leo kuachana na kile ilichotaja kuwa "hatua za uharibifu", baada ya zaidi ya ndege 100 za kivita na meli tisa za jeshi la wanamaji za China kuripotiwa katika maeneo yaliyo karibu na kisiwa hicho kinachojitawala.

 Wizara ya ulinzi ya Taiwan imesema idadi ya ndege za kivita zilizoripotiwa ndani ya saa 24 ni kubwa mno huku Beijing hadi sasa ikijizuia kuelezea chochote juu ya tukio hilo.

Hatua hizo huenda ikawa jaribio la kuathiri matokeo ya uchaguzi wa rais unaotarajiwa mwezi Januari mwaka ujao.

China inawapigia upatu wagombea wa upinzani wenye dhamira ya kushirikiana na Beijing kuliko wale wa chama tawala cha DPP ambao sera yao inajikita katika uhuru kamili wa kisiwa hicho.

China inadai kuwa kisiwa cha Taiwan ni eneo lililo chini ya himaya yake na iwapo italazimika itakitwaa kwa nguvu. Beijing imekuwa ikiongeza shinikizo la kidiplomasia na kijeshi kwa Taipei katika miaka ya hivi karibuni.