Spika wa bunge Tanzania asema wabunge wa viti maalum ni halali | Matukio ya Afrika | DW | 30.11.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Spika wa bunge Tanzania asema wabunge wa viti maalum ni halali

Spika wa bunge la Tanzania Job Ndugai, asema wabunge 19 walioteuliwa na chama cha CHADEMA kwa ajili ya viti maalumu na kisha kuapishwa ni wabunge halali isipokuwa wao wenyewe waamue vinginevyo. 

Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Yustin Ndugai, ametoa tahadhari kwa mtu yoyote atakayelidhalilisha bunge hilo na kwamba wabunge 19 walioteuliwa na chama cha CHADEMA kwa ajili ya viti maalumu na kisha kuapishwa ni wabunge halali isipokuwa wao wenyewe waamue vinginevyo. 

Kauli hiyo ya spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Yustin Ndugai, ameitoa hii leo mjini Dodoma mara baada kumaliza kuwaapisha wabunge wawili walioteuliwa na Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli. Wabunge hao ni Hamphrei Polepole na Riziki Lulida.

Tansania Dodoma | Parlamentsmitglieder der Oppositionspartei CHADEMA

Kuna sintofahamu kuhusu kuhusu wabunge wa viti maalum

Akizungumza mara baada ya kuwaapisha wabunge hao, Spika Ndugai amesema kuwa kuna baadhi ya watu wamejipambanunua kwa kukejeli shughuli za bunge na kuwatahadharisha kwa kusema kuwa ni jambo lisilokubalika kwa mtu yeyote kudharau shughuli za bunge na hata kuwadhalilisha wabunge waliokwisha kuapishwa wakiwemo wabunge 19 wa viti maalumu wa chama cha CHADEMA walioapishwa hivi karibuni na kuongeza kuwa.

Kwa upande wao wabunge walioteuliwa na Rais katika nafasi zake kumi za uteuzi wamesema kuwa watailinda katiba ya nchi kwa kuwatumikia Watanzania, kama anavyosema mbunge Riziki Lulida akifuatiwa n Hamphrei Polepole ambaye pia ni katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi CCM

Hafla hiyo ya wabunge wateule wa Rais Magufuli imefanyika katika viwanja vya bunge mjini Dodoma na kuhudhuria na katibu wa bunge hilo pamoja na wafanyakazi wa bunge hilo na kwamba wabunge wote walioapishwa tayari ni wabunge na kwamba wanaanza shughuli za kibunge mara moja.

Hata hivyo wakati spika wa bunge Job Yustin Ndugai akipigilia msumari kuendelea kuwatambua wabunge 19 wa viti maalumu kutoka chama cha Chadema licha ya kwamba tayari kamati kuu ya chama hicho iliyoketi hivi karibuni alichukua uamuzi wa kuwafutia uanachama wabunge hao wakiongizwa na aliyekuwa mbunge wa Kawe Halima Mdee.

Deo Kaji Makomba - DW Dodoma