Spika Uganda aunga mkono shindano la wanawake wanene | Matukio ya Afrika | DW | 27.02.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Spika Uganda aunga mkono shindano la wanawake wanene

Shindano la uembo la wanawake wanene au wenye maumbo makubwa nchini Uganda limepata uungwaji mkono kutoka kwa spika wa bunge la nchi hiyo. Baadhi ya viongozi katika jamii wamekosoa lengo la shindano hilo.

Mabishano kuhusu mashindano ya wanawake wanene walio na maumbo ya kipekee Uganda yamechukua mkondo mwingine baada ya spika wa bunge la nchi hiyo kubadili msimamo wake na kuamua kuyaunga mkono. Hii ni baada ya wandalizi na washiriki katika mashindano hayo kuwasilisha ufafanuzi wao kwake.

Tofauti na madai kwamba wanalenga kuyatumia kuwa kivutio cha watalii, wanasema kuwa kupitia kwa mashindano yao wanalenga kuondosha unyanyapaa miongoni mwa wenzao walio na maumbo ya kipekee wafahamu kuwa nao ni warembo.

Miongoni mwa hoja zao za kuandaa mashindano hayo ni kuiwezesha jumuiya wanawake hao Uganda na barani Afrika kuondokana na unyanyapaa na kujiamini kwamba hata nao ni warembo. Hii kwa mtazamo wao itaondosha fikra za kimagharibi kuwa urembo unamaanisha mtu kuwa mwembamba. .

Spika wa bunge ambaye siku mbili zilizopita alipinga vikali mashindano hayo akisema kuwa hatakubali wanawake wa Uganda kudhalilishwa kama vivutio kwa watalii, amebadili msimamo wake baada ya kupokea ufafanuzi huo akasema.

Washiriki wamesema lengo la mashindano hayo ni kuwawezesha wanawake hao wenye maumbo makubwa Uganda na barani Afrika kuondokana na unyanyapaa na kujiamini kwamba hata nao ni warembo.

Washiriki wamesema lengo la mashindano hayo ni kuwawezesha wanawake hao wenye maumbo makubwa Uganda na barani Afrika kuondokana na unyanyapaa na kujiamini kwamba hata nao ni warembo.

Tangu mashindano hayo yalipozinduliwa mapema mwezi huu, wanasiasa,wanaharakati wa haki za wanawake na viongozi wa kidini wamejitokeza na kuyashtumu vikali huku wakimtaka waziri wa nchi wa utalii ajiuzulu kwa kuongoza katika kuwavunjia wanawake hadhi na heshima yao. 

Hadi sasa zaidi ya washiriki 200 kutoka sehemu mbalimbali za Uganda pamoja na nchi jirani ya Rwanda wamejisajili kushiriki. Mshiriki anatakiwa kuwa kati ya umri wa miaka 18 hadi 35.Kwa mujibu wa ufafanuzi wao, waandalizi wa Miss Curvy Uganda wanasisitiza kuwa watachangia katika kuondosha unyanyapaa miongoni mwao.

Kulingana na waandalizi wa mashindano hayo, Uganda si nchi ya kwanza kuandaa mashindano hayo.Yamefanyika Nigeria na kwingineko kama mashindano yoyote yale ya mitindo na urembo lakini yakiwahusisha tu wanawake walio na miili minene. Kuna makundi ya watu ambao tayari wamewasilisha shauri mahakamani kupinga mashindano hayo ambayo yamepangwa kuyanyika mwezi Aprili mwaka huu.