Somalia yaahirisha uchaguzi wa urais kwa mara ya nne | Matukio ya Afrika | DW | 27.12.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Somalia yaahirisha uchaguzi wa urais kwa mara ya nne

Somalia imeahirisha uchaguzi wa urais kwa mara ya nne huku kukiwa na madai ya udangayifu na vitisho.

Kura ya urais ilipangwa kufanyika tarehe 28 Desemba. Lakini afisa wa tume ya uchaguzi amewaeleza wanahabari kuwa tarehe mpya ya uchaguzi huo itakuwa ni mwishoni mwa mwezi Januari, wakati nchi hiyo itakapowachagua wabunge wenye jukumu la kumchagua rais. Rais nchini Somalia hachaguliwi moja kwa moja kwa kura za wananchi. Wanachama wa upinzani wamekuwa na wasiwasi juu ya kucheleweshwa kwa uchaguzi huo kwa muda mrefu, wakisema mchakato umeathiriwa na udanganyifu unaotaka kukipendelea chama tawala.

Matangazo

IJUE DW

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com