1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sheinbaum atarajiwa kushinda uchaguzi Mexico

3 Juni 2024

Mgombea wa serikali Claudia Sheinbaum anatarajiwa kushinda uchaguzi wa rais nchini Mexico.

https://p.dw.com/p/4gYfF
Mexiko | Wahlkampf von Claudia Sheinbaum
Picha: Hector Vivas/Getty Images

Haya ni kulingana na tafiti zilizofanyiwa wapiga kura na gazeti la kibiashara la El Financiero na shirika la utangazaji la Televisa, baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa usiku wa kuamkia leo.

Akiwa ni rafiki wa karibu wa rais aliye madarakani Andres Manuel Lopez Obrador, huenda Sheinbaum kutoka chama tawala cha mrengo wa kushoto cha Morena, akawa rais wa kwanza wa kike kuitawala Mexico, iwapo atachaguliwa.

Mpinzani wake mkuu ni Xochitl Galvez, mgombea ambaye anaungwa mkono na muungano mkubwa wa vyama vitatu vya upinzani. Mgombea watatu Jorge Alvarez Maynez kutoka chama kimoja kidogo, anaonekana kutokuwa na nafasi ya kushinda uchaguzi huo.