1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz azungumza na rais Aliyev kuhusu Nagorno-Karabakh

5 Oktoba 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amehimiza kuwepo amani ya kudumu na suluhu kupitia mazungumzo, katika mzozo kati ya Azerbaijan na Armenia juu ya eneo linalozozaniwa la Nagorno-Karabakh.

https://p.dw.com/p/4X7mO
Berlin Kanzler Scholz und Aserbeidschan Präsident Alijew
Picha: Christian Spicker/IMAGO

Kulingana na naibu msemaji wa serikali ya Ujerumani Christiane Hoffmann, Scholz alizungumza kwa njia ya simu na Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev jana Jumatano, na kumueleza kuwa anapinga vikali matumizi ya nguvu za jeshi na kusisitiza umuhimu wa kuwepo uwazi juu ya mzozo huo.

Hivi majuzi  Rais Aliyev alikataa mwaliko kutoka kwa viongozi wa Umoja wa Ulaya wa kukutana hii leo na Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan pembezoni mwa mkutano wa Jumuiya ya Kisiasa ya Ulaya (EPC) huko Grenada, Uhispania.

Viongozi wa Ulaya walitarajia mkutano huo ungetoa nafasi ya kupatanisha mzozo huo.

Azerbaijan ilichukua udhibiti kamili wa jimbo la Nagorno-Karabakh baada ya kuendesha operesheni kubwa ya kijeshi mwezi uliopita, na tangu wakati huo, zaidi ya watu 100,000 wamekimbia eneo hilo kuelekea Armenia na hivyo kuzusha mzozo mkubwa wa kibinaadamu.