1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Frank Habineza bado ana matumaini ya kugombea urais Rwanda

18 Machi 2024

Licha ya vitisho vya kuuawa na kufungwa gerezani na kutokuwepo kwa usawa nchini Rwanda, Frank Habineza ambaye ni kiongozi wa upinzani nchini humo bado ana matumaini ya kugombea tena urais kupambana na Rais Kagame.

https://p.dw.com/p/4dsFl
Rwanda l 2010 Afrika/  Kigali
Rwanda inatarajia kufanya uchaguzi wake mkuu Julai mwaka huuPicha: picture-alliance/dpa

Nchini Rwanda, Mpinzani wa kisiasa wa rais Kagame, Frank Habineza amepokea vitisho vya kuawa, kufungwa gerezani na kulazimishwa kwenda uhamishoni, Na yote haya yanatokana na jaribio lake la kuwania urais nchini humo, Na licha ya kutokuwepo kwa usawa, kiongozi huyo wa upinzani bado ana matumaini ya kugombea tena urais.

Soma zaidi.  Dkt Habineza: Kagame kabidhi madaraka, fuata katiba

Akizungumza na shirika la habari la AFP, Frank Habineza, Kiongozi wa upinzani nchini Rwanda amesema umefika wakati sasa wa kuacha siasa za kuzungumza ndani za bila vitendo na kuingia uwanjani kubadilisha mambo.

Frank Habineza amesema "Inabidi tuendelee kupambana kwa sababu hili jambo la demokrasia huwezi kulifanya ukiwa umejiweka pembeni. Kwa hapa Ufaransa tuna kitu tunakiita 'siasa za kujikunyata kitini yaani juhudi zako hazibadilishi chochote kutokana na kujiweka kwako pembeni. Unahitaji kuwemo ndani ya siasa. Unahitaji kupambana ukiwa mchezoni hapo ndio unaweza kubadilisha kitu. Amini katika hilo."

Uchaguzi mkuu Rwanda kufanyika Julai 15 mwaka huu


Taifa hilo la Afrika Mashariki litafanya uchaguzi wa rais na wabunge Julai 15 mwaka huu, huku Kagame akitarajiwa kuendeleza utawala wake katika nchi ambayo ameiongoza kwa takriban robo karne.

Rwanda / Paul Kagame
Rais wa Rwanda Paul KagamePicha: Trinidad Express Newspaper/AFP

Kagame, mwenye umri wa miaka 66 alikua rais wa Rwandatangu mwezi Aprili 2000 lakini amekuwa kiongozi mkuu wa nchi hiyo tangu mwisho wa mauaji ya kimbari ya 1994, alirejea tena madarakani kwa ushindi wa kishindo kwa zaidi ya asilimia 90 ya kura katika chaguzi za 2003, 2010 na 2017.

Soma zaidi.  Frank Habineza- sauti adimu ya ukosoaji Rwanda

Kwa upande wake, Habineza alipata asilimia 0.45 pekee ya kura katika uchaguzi wa 2017, akishika nafasi ya tatu katika uchaguzi ambao makundi ya kutetea haki za binadamu yalikosoa kutokana na ukiukwaji wa sheria na vitisho kwa wapiga kura.

Mara hii tena Frank Habineza anasema "Ninagombea urais kwa sababu bado naamini kuwa Rwanda inahitaji kuwa na demokrasia yenye nguvu zaidi. Nchi yetu haina demokrasia sana, ilikosa uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kujieleza. Bila shaka , kwa hiyo hayo ndiyo mambo ambayo tutayazingatia, lakini bila shaka kama chama cha siasa tunaamini pia katika kuondoa umaskini."

Habineza: Bado safari ni ndefu kisiasa Rwanda


Chama cha Habineza cha Green Party kilichosajiliwa mwaka 2013 ndicho chama pekee cha upinzani nchini Rwanda kilichoruhusiwa na kilishinda viti viwili bungeni kwa mara ya kwanza mwaka wa 2018 huku vyama vingine vya upinzani vilivyosajiliwa vikiwa vinamuunga mkono Kagame.

Kiiongozi huyo wa upinzani anaongeza kuwa bado yapo masuala chungu nzima yanayoididimiza demokrasia nchini Rwanda.

 “Nasema bado tuna changamoto za uhuru wa kujieleza, watu bado hawana uhuru wa kujieleza wanavyotaka kwa sababu wanaogopa madhara, bado kuna masuala ya uhuru wa vyombo vya habari. unaona kuna baadhi ya waandishi wa habari wapo gerezani kwa mambo fulani ambayo wasingefungwa kwa sababu hiyo.Na hata kuna tuhuma za kuteswa gerezani kwa waandishi hawa, nadhani umewahi kusikia mmoja wao ni anaitwa Cyuma, nadhani Hassan, ameteswa gerezani, sasa anazidi kupata upofu amesema Habineza.

Ruanda Victoire Ingabire Oppositionsführerin
Mpinzani wa siasa nchini Rwanda, Victoire IngabirePicha: STEPHANIE AGLIETTI/AFP

Kwa upande mwingine, Mpinzani mwingine pekee aliyetarajiwa kumtia joto Kagame ni Victoire Ingabire, kiongozi wa vuguvugu lisilosajiliwa la Dalfa Umurunzi,Yeye amezuiwa kwenye kinyang'anyiro cha urais kutokana na kutiwa hatiani hapo awali, Ingawa maamuzi wa mahakama kuhusu iwapo ataruhusiwa kugombea urais umepangwa Machi 13.

Soma zaidi. Kagame ashinda kwa kishindo uchaguzi Rwanda

Kiongozi huyo alikamatwa mwaka 2010 akiwa kwenye kampeni za kumpinga Kagame, Ingabire alipatikana na hatia ya uhalifu akitajwa kuleta "mgawanyiko" baada ya kuhoji hadharani maelezo ya serikali ya mauaji ya kimbari ya 1994 yaliyolenga Watutsi ambayo yaliua takriban watu 800,000.

Hata hivyo, Frank Habineza ambaye awali alikuwa mwanachama wa chama tawala cha Kagame kabla ya kuhama mwaka 2009 ana matumaini kwamba atawavutia wapiga kura wengi kwa kuja na mpango unaolenga kuimarisha haki za binadamu na uhuru wa kujieleza.


Lakini pamoja na mikakati hiyo wakosoaji wanadai kuwa ni lazima kiongozi huyo wa upinzani  aondoe shutuma kutoka kwa baadhi ya waangalizi kwamba kugombea kwake kuna maana ndogo na ni kwa matakwa ya kuwaridhisha wafadhili wake wa mataifa ya Magharibi.