RAMALLAH: Mashambulizi kusitishwa na badala yake hawatosakwa | Habari za Ulimwengu | DW | 15.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

RAMALLAH: Mashambulizi kusitishwa na badala yake hawatosakwa

Idadi kadhaa ya wanamgambo wa kundi la Fatah kwenye Ukingo wa Magharibi wameahidi kutofanya mashambulio dhidi ya Israel kwa ahadi kuwa Israel nayo itaacha kuwasaka.Maafisa wa Israel wamesema, makubaliano hayo yatatoa msamaha kwa kiasi ya wanamgambo 180 wa Fatah.Wanamgambo hao watajiunga rasmi na vikosi vya usalama vya Kipalestina. Israel kwa upande wake itawatoa Wapalestina hao kutoka orodha ya wanamgambo wanaosakwa. Makubaliano hayo ni sehemu ya ishara zitakazoonyeshwa na waziri mkuu Ehud Olmert wa Israel atakapokutana na Rais wa Wapalestina, Mahmoud Abbas siku ya Jumatatu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com