Rais wa Iran aomba radhi kwa mauaji ya waandamanaji
11 Februari 2026
Matangazo
Shinikizo zaidi zinatoka kwa raia wanaolaani mauaji yaliyofanyika wakati wa maandamano nchini humo.
Televisheni ya kitaifa imeonesha makumi kwa maelfu ya watu kote nchini humo wakihudhuria mikutano ya kuiunga mkono serikali, huku wengine wakizichoma bendera za Marekani na kutaka "kuangamizwa kwa Marekani."
Wakati huo huo, Rais Masoud Pezeshkian amesema Iraniko tayari kufanya majadiliano kuhusu mpango wake wa nyuklia wakati ambapo mazungumzo ya nchi hiyo na Marekani yakiwa hayajapata mwafaka.
Akizungumzia maandamano na mauaji yaliyofanyika nchini humo hivi majuzi ingawa si moja kwa moja, Pezeshkian amesema máuaji hayo yalisababisha huzuni kubwa.