1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Rais wa Iran aagiza mazungumzo ya haki na usawa na Marekani

3 Februari 2026

Rais wa Iran Masoud Pezeshkian amemuagiza Waziri wa Mambo ya Nje Abbas Araghchi kufanya "mazungumzo ya haki na usawa" na Marekani.

https://p.dw.com/p/57yQ1
Iran Tehran 2026 | Rais Masud Pezeshkian katika kumbukumbu ya Ayatollah Ruhollah Khomeini, mwanzilishi wa Mapinduzi ya Iran.
Rais wa Iran Masoud Pezeshkian akihudhuria sherehe iliyofanyika katika kaburi la Ayatollah Ruhollah Khomeini, mwanzilishi wa Mapinduzi ya Iran, kusini mwa Tehran, katika maadhimisho ya miaka 47 ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran mnamo Januari 31, 2026.Picha: Iranian Presidency/Anadolu/picture alliance

Pezeshkian amesema kupitia mtandao wa X kwamba amemuagiza Araghchi kufanya mazungumzo hayo kwa kuongozwa na misingi ya utu, busara, na uthabiti, lakini kwa kuzingatia mazingira yanayofaa, yasiyokuwa na vitisho na matarajio yasiyo na msingi.

Aidha ameagiza kwamba mazungumzo hayo "yafanyike ndani ya mfumo wa maslahi ya taifa hilo."

Kulingana na vyombo vya habari vya Marekani, Araghchi anatarajiwa kufanya mazungumzo ya nyuklia na mjumbe maalumu wa Marekani Steve Witkoff mjini Istanbul siku ya Ijumaa.

Hata hivyo Wairan wengi wanapinga vikali makubaliano na Marekani, wakihisi kama wamesalitiwa na Rais Donald Trump aliyeahidi kuwasaidia waandamanaji wanaoipinga mamlaka nchini humo.