SiasaBurundi
Rais wa Burundi ateuliwa na chama chake kuwania Urais 2027
27 Aprili 2026
Matangazo
Ndayishimiye mwenye umri wa miaka 57, ameiongoza Burundi tangu mwaka 2020, akichukua nafasi hiyo baada ya kuchaguliwa na kufuatia kifo cha mtangulizi wake Pierre Nkurunziza na atagombea kwa muhula mwingine wa miaka saba.
Rais Evariste Ndayishimiye ambaye aliteuliwa Jumapili, amekishukuru chama chake kwa kumwamini na akaahidi kuendeleza sera na mipango kwa ajili ya maendeleo ya Burundi. Hata hivyo rais huyo anatazamiwa kuibuka mshindi huku upinzani wakisema kuwa uchaguzi huo hautakuwa wa huru na haki.
Epitace Nshimirimana, msemaji wa chama cha upinzani kilichopo uhamishoni cha MSD ameukosoa utawala wa Ndayishimiye akisema umeshindwa kutafutia jawabu suala la uhaba wa mafuta, fedha za kigeni na mahitaji ya msingi ya raia.