1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Pierre Nkurunziza

Pierre Nkurunziza ni mwanasiasa wa Burundi ambaye amekuwa rais tangu mwaka 2005. Alikuwa mwenyekiti wa Baraza la Taifa la kutetea demokrasia - Vikosi vya kutetea demokrasia - CNDD-FDD - Chama tawala nchini Burundi.

Mwaka 2015 Nkurunziza aliteuliwa kiutata na chama chake kuwania muhula wa tatu madarakani. Wafuasi na wapinzani wa Nkurunziza walitofautiana juu ya iwapo ilikuwa halali kwake kugombea tena, na mandamano yakafuatia. Maandamano ya kumpinga Nkurunziza yaliyodumu kwa zaidi ya miezi miwili, ambayo yalikuwa yanakandamizwa vibaya, yalisababisha vifo vya watu zaidi ya 100. Mei 13, 2015 jaribio la mapindizi dhidi ya Nkurunziza lilitokea wakati akiwa hayupo nchini, kiongozi wa jaribio hilo Godefroid Niyombare, alidai kumpindua Nkurunziza, inagawa maafisa wake watiifu walikanusha hilo. Yakikabiliwa na upinzani kutoka vikosi tiifu kwa Nkurunziza, mapinduzi hayo yalishindwa na vikosi tiifu vilirejesha udhibiti kamili kufikia Mei 15. Vyombo huru vya habari vilifungiwa na wapinzani walitoroka, na kuungana na Warundi wengine wapatao 150,000. Baada ya uchaguzi kususiwa na upinzani, Nkurunziza alichaguliwa kwa muhula wa tatu Julai 2015.

Onesha makala zaidi